Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2018

Tapeli ahukumiwa kifungo cha miaka 13,275 jela Thailand

Mahakama moja ya Thailand imemuhukumu tapeli mmoja zaidi ya kifungo cha miaka 13,000 jela. Pudit Kittithradilok ,34, alikiri kumiliki mradi mmoja wa piramidi ambao aliwaahiidi wawekezaji kupata mapato ya hali ya juu. Takriban watu 40,000 walikubali kuwekeza kiwango cha $160m katika kampuni yake. Mahakama ilisema kuwa alijihusisha na vitendo vya kutoa mikopo na makosa 2,653 ya udanganyifu. Baada ya kukiri ,mahakam hiyo ilipunguza hukumu hiyo na kumpatia kifungo cha miaka 6,637 na miezi sita. Huenda asihudumu zaidi ya miaka 20 kwa kuwa sheria ya Thai inatoa miaka 10 kwa makosa mawili aliyopatikana nayo. Waendesha mashtaka waliambia mahakama kwamba Pudit aliandaa semina ambapo waliohudhuria walishawishiwa kuwekeza katika kile alichosema ni biashara zinazohusiana na ujenzi ,urembo, uuzaji wa magari yaliotumika uuzaji wa bidhaa nje ya nchi miongoni mwa vitu nyengine. Kulingana na gazeti la Bangkok Post, wawekezaji waliahidiwa mapato makubwa na marupurupu iwapo wataleta wan...

Tundu Lissu aitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati Tanzania

‎ Mnadhimu mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema Bw Tundu Lissu amesema dalili zinaonesha watu waliomshambulia kwa risasi mjini Dodoma mwaka jana walikuwa na uhusiano na serikali. Bw Lissu, akihutubia wanahabari kwa mara ya kwanza tangu kulazwa hospitalini, ameonekana kuilaumu serikali ya Rais John Magufuli kwa kuwakandamiza wapinzani. Amesema anaamini shambulio dhidi yake lililenga kumnyamazisha kutokana na uokosoaji wake wa mara kwa mara wa serikali. Bw Lissu alikuwa akihutubu kutoka hospitali ya Nairobi jijini Nairobi ambapo amekuwa akipokea matibabu kwa miezi minne sasa. Mbunge huyo wa Singida Mashariki ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati akisema hali nchini Tanzania imebadilika sana. Bw Lissu amesema kufikia sasa anaamini hakuna uchunguzi wa maana kuhusu kushambuliwa kwake mnamo 7 Septemba unaendelea. Aidha, amesema Rais John Magufuli, ingawa aliandika ujumbe kwenye Twitter na pia kumtuma makamu wake Samia Suluhu Hassan, hajawahi kuzungu...