Skip to main content

Tundu Lissu aitaka jamii ya kimataifa kuingilia kati Tanzania


Mnadhimu mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema Bw Tundu Lissu amesema dalili zinaonesha watu waliomshambulia kwa risasi mjini Dodoma mwaka jana walikuwa na uhusiano na serikali.
Bw Lissu, akihutubia wanahabari kwa mara ya kwanza tangu kulazwa hospitalini, ameonekana kuilaumu serikali ya Rais John Magufuli kwa kuwakandamiza wapinzani.
Amesema anaamini shambulio dhidi yake lililenga kumnyamazisha kutokana na uokosoaji wake wa mara kwa mara wa serikali.
Bw Lissu alikuwa akihutubu kutoka hospitali ya Nairobi jijini Nairobi ambapo amekuwa akipokea matibabu kwa miezi minne sasa.
Mbunge huyo wa Singida Mashariki ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati akisema hali nchini Tanzania imebadilika sana.
Bw Lissu amesema kufikia sasa anaamini hakuna uchunguzi wa maana kuhusu kushambuliwa kwake mnamo 7 Septemba unaendelea.
Aidha, amesema Rais John Magufuli, ingawa aliandika ujumbe kwenye Twitter na pia kumtuma makamu wake Samia Suluhu Hassan, hajawahi kuzungumzia hadharani kisa cha kushambuliwa kwake.
"Tanzania imebadilika na kuwa taifa ambalo hakuna aliye salama. Mawakili wanaweza kurushiwa mabomu kwa kuwawawkilisha wateja wao. Nchi ambayo afisi za mawakili zinaweza kuvamiwa, na mawakili kufungwa jela," amesema Lissu.
Bw Lissu amesema amepona na kwamba anashukuru Mungu na wote waliomtakia uponaji wa haraka.
CHANZO BBC SWAHILI

Comments

Popular posts from this blog

TIGO HAND SET CONFIGURATION - KUUNGANISHA INTERNANT KWENYE SIMU

Kuunganisha internet kwenye sim inategemea na simu yenyewe,ni aina gani na mfumo wake ni upi? ->>kina aina nyingi za simu lakini baadhi unaweza kuzigawa katika makundi ma nne (4) 1. SMART PHONE 2. BLACK BERRY 3. IPHONE ( IPOD ) 4. NORMAL               1. ANDROID Simu za android unaweza kuziweka katika makundi mawili kutegemea na SETTING ZAKE -Tofauti ya hizi ni maneno WIRELESS and NETWORK na MORE NETWORK. >>JINSI YA KUSETI ANDROID (Njia ya kwanza ) Bonyeza MENU Nenda kwenye SETTING Kisha ingia WIRELESS AND NETWORK  Kisha ingia MOBILE NETWORK Nenda  ACCESS POINT NAME ( APN ) Nenda ADD NEW    Name andika TIGOWEB APN andika  TIGOWEB Authentication type weka  CHAP SAVE NJI YA PILI Bonyeza MENU Nenda kwenye SETTING Kisha ingia kwenye MORE SETTING Halafu nenda (MOBILE NETWORKS  Nenda ACCESS POINT NAME (APN) Nenda kwenye ADD   Name andika ( TIGOWEB ) APN ...

TIGO GAWIO

 TIGO NI KAMPUNI YA KWANZA DUNIANI KUGAWA FAIDA KWA WATEJA WAKE. Gawio ni huduma ya tigo inayompatia mteja wetu faida ya matumizi yake ya tigo pesa kwa kila miezi mi tatu.      Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo kuhusu kutoa gawio la kiasi cha shilingi bilioni 14.25 lililolimbikizwa kwenye akaunti ya mfuko wa fedha wa Tigo Pesa kwa ajili ya wateja wao. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Tigo Pesa Andrew Hodgson na Meneja Masoko na Usambazaji wa Tigo Pesa Catherine Rutenge (kulia).     Mkuu wa Idara ya Tigo Pesa Andrew Hodgson akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu gawio la shilingi bilioni 14.25 litakalo anza kutolewa kwa wateja wa kampuni hiyo. Gawio hili litawanufaisha jumla ya watumiaji milioni 3.5 wa Tigo Pesa nchini. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez. Tigo Tanzania leo imetangaza itatoa gawio la kiasi cha s...

TIGO SHOP / NAMBA YA MAAJABU / NAMBA YA VIFURUSHI

ULIPO TUPO TIGO SHOP / NAMBA YA MAAJABU / NAMBA YA KUJIUNGA VIFURUSHI   TIGO SHOP / NAMBA YA MAAJABU / NAMBA YA KUJIUNGA  >>Tigo shop Menu *148*00#    -Ni namba ambayo inakupa mteja vifurushi mbalimbali vya kutuma SMS ,INTERNET, Pamoja na sms. ->itakupa vifurushi vifuatavyo ->>OFA Maalum (kifureshi namba moja) -Internet BURE     ,Kifurushi hiki kitakupa bure MB 100 Bilakikomo cha spidi kutumia kati ya saa 12 ASUBUHI mpaka   saa   2 ASUBUHI: BILA KULIPIA -MIA MIA Bilakikomo     Ndugu mteja utaongea bila kikomo TIGO -TIGO Na utalipia sh 100 kwa kila simu uipigayo,KUJIUNGA NI BURE -USIKU Bilakikomo (GB 30 ) =Sh 1,000   kifurushi hiki kinakupa GB 30 Bila kikomo cha spidi,mteja Utatumia kati ya saa 5 usiku Hadi sdaa 11 Asubuhi Na kitadumu kwa muda wa siku 2 MFULULIZO Kwa shilingi 1,000 tu.  - 999 sh = 900 min + 500 SMS      Ki...