TIGO NI KAMPUNI YA KWANZA DUNIANI KUGAWA FAIDA KWA WATEJA WAKE. Gawio ni huduma ya tigo inayompatia mteja wetu faida ya matumizi yake ya tigo pesa kwa kila miezi mi tatu.
Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo kuhusu kutoa gawio la kiasi cha shilingi bilioni 14.25 lililolimbikizwa kwenye akaunti ya mfuko wa fedha wa Tigo Pesa kwa ajili ya wateja wao. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Tigo Pesa Andrew Hodgson na Meneja Masoko na Usambazaji wa Tigo Pesa Catherine Rutenge (kulia).
Mkuu wa Idara ya Tigo Pesa Andrew Hodgson akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu gawio la shilingi bilioni 14.25 litakalo anza kutolewa kwa wateja wa kampuni hiyo. Gawio hili litawanufaisha jumla ya watumiaji milioni 3.5 wa Tigo Pesa nchini. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez.

Tigo
Tanzania leo imetangaza itatoa gawio la kiasi cha shilingi bilioni
14.25 (sawia na dola za kimarekani bilioni 8.7) lililolimbikizwa kwenye
akaunti yake ya mfuko wa fedha wa Tigo Pesa kwa ajili ya wateja wake.
Hii inaifanya kampuni hiyo kuwa mtandao wa simu ya kwanza duniani kutoa
gawio la fedha kutokana na huduma ya kutuma na kutoa fedha.
Akaunti
ya mfuko wa fedha wa Tigo Pesa (Tigo Pesa Trust Account) ni akaunti
ambayo fedha zote za Tigo Pesa zinakusanywa na kuhifadhiwa toka huduma
ya Tigo Pesa ilipoanza miaka mine iliyopita. Kwa sasa Tigo ipo tayari
kutoa gawio la fedha hizo ambazo zilikuwa zinazaa faida baada ya
kuridhiwa na Benki Kuu ya Tanazania (BOT) kwa barua rasmi ya
kutokuwa na pingamizi iliyopokelewa Julai mwaka huu.
Meneja
Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kwamba gawio hilo la faida
itawanufaisha wateja wote wa Tigo, wakiwemo mawakala wakuu, mawakala wa
reja reja na mteja mmoja mmoja, mtumiaji wa Tigo Pesa.
“Kwa
miaka mitatu na nusu sasa mfuko wa fedha wa Tigo Pesa ulikuwa
ukikusanya faida kwa kiwango cha asilimia 5 hadi 12, na mpaka Juni mwaka
huu faida hiyo imefikia shilingi bilioni 14.25. Lengo ni kuwapatia
wadau wetu wa Tigo Pesa fursa ya kupata faida kutokana na kiasi cha
fedha walichoweza kukiweka katika akaunti zao za Tigo Pesa,” alisema
Gutierrez.
Aliongeza,
“Wastani ya faida ambayo mteja yeyote ataweza kupata inatofautiana na
wastani wa fedha ambayo ataweza kubaki nayo kwenye akaunti yake ya Tigo
Pesa kwa siku. Kwa hivyo viwango vya faida vitatofautiana kati ya wakala
mkuu, wakala wa reja reja au mteja wa kawaida.”
Gawio
hili litawanufaisha jumla ya watumiaji milioni 3.5 wa Tigo Pesa nchini,
wakiwemo mawakala wakuu na mawakala wa reja reja ambao wana umuhimu wa
kipekee kwenye muundo mzima wa mtandao wa huduma ya kutuma na kupokea
pesa nchini Tanzania.
“Ukiondoa
kiasi cha dola milioni 100 za kimarekani ambazo tulikuwa tumeahidi
kuendelea kuwekeza nchini kila mwaka kama mpango moja wapo wa kuongeza
ufanisi katika mtandao wetu, gawio la mfuko wa fedha wa Tigo Pesa ni
uwekezaji wa moja kwa moja kwa maisha ya Watanzania, kwa sababu
itasaidia kuinua kiwango cha kipato na hali za kiuchumi kwa wateja wetu.
Pia ni udhibitisho kwamba kampuni yetu inaendelea kuwajibika katika
kuwajumuisha wananchi katika mzunguko wa fedha na kiuchumi kwa kupanua
wigo wa matumizi ya Tigo Pesa kote nchini,” alisema Gutierrez
Comments
Post a Comment